Unaweza kujiajiri kupitia kilimo cha bustani kwa kulima mazao ya mbogamboga kama vitunguu ,nyanya .bamia . nyanya chungu na nk
KILIMO CHA VITUNGUU
kilimo cha vitunguu ni fursa kubwa ya mafanikio kutokana na faida kubwa inayopatikana katika zao hilo .
Vitunguu hustawi maeneo yasiyokua na mvua nyingi baridi kiasi udongo usio tuamisha maji joto la wastani kwa hapa Tanzania maeneo yanayofaa kufanya kilimo cha vitunguu ni Morogoro. Singida. Arusha. Iringa Pwani Kilimanjaro
Atua za kufatwa kwenye kilimo cha vitunguu
kuandaa kitalu cha kusia mbegu
kitalu kiandaliwe kwa usafi na kutiwa mbolea ya asili kisha kusia mbegu kwa mstari zisibanane sana zikibanana sana azitanenepa na zitachelewa kua tayar kwenda shamba
Kuanda majoruba kwajili ya kupanda vitunguu
maandalizi ya shamba la kupandia yanatakiwa yafanyike mapema yaandaliwe majoruba ambayo yataifadhi maji kama ni kipindi cha kiangaz yaandaliwe kwa mpangilio kwa kutumia kamba ili maji yaweze kutembea katika shamba zima katika kila joruba itiwe samadi debe moja ichanganywe na udongo
KUPANDA VITUNGUU
mbegu zitadumu kwenye kitalu kwa siku 40 zikisha kua tayar zitahamishiwa shambani zipandwe kwa mpangilio(mstari) katika majuruba wakati shamba likiwa limelowa maji ili mmea usizohofike
Baada ya wiki mbili itaitajika mbolea ya kukuzia mmea wa kitunguu pamoja na booster ya majani dawa ya wadudu Atakan na dawa ya ukungu dawa itanyunyuziwa kwa wiki mara mbili
Baada ya siku 90 vitunguu vitakua tayar majan yataanza kukauka shamban patanyweshewa mara moja kabla ya kuvuna na baada ya hapo vitunguu vitangolewa kwa utaratibu kwa kutumia vijembe vidogo au kisu vikasha ngolewa vitakatwa shingo vikashwe siku mbil juan baada ya hapo vitunguu vitakua tayar kwa kuuzwa au kutumika
BEI YA VITUNGUU
vitunguu hufukia hadi 200000 kama wakulima hawakua wengi katika msimu kiwango cha chini cha bei ya vitunguu na 60000 kwa kilo mia wakulima wakiwa wengi na zao linaloweza kukufanya ujiajiri na kuachana na MAMBO YA MSINGI
Mtaji
Eneo
Usimamizi
Maji
WAZA KWA NGUVUUUU UTATOKAAAA