
Wanajeshi wa Kenya wanasema wamedhibiti jengo la Westgate
Vikosi vya usalama nchini Kenya
vinasema viko katika mkondo wa lala salama katika kuweza kudhibiti jengo
zima la Westgate. Hadi sasa serikali inasema kuwa mateka wote
wameokolewa huku wanamgambo sita waliosalia wakiuawa usiku wa kuamkia
leo.
Kwa mujibu wa taarifa za maafisa wa usalama idadi kamili ya magaidi waliouawa ni tisaInaarifiwa magaidi hao walijitawanya wakiwa ndani ya jengo hilo kila mmoja akijificha sehemu yake katika ghorofa ya juu zaidi ya jengo hilo.
Milio ya risasi na milipuko ilisikika mapema leo asubuhi kutoka katika jengo hilo.
Ukabilianaji huo ulitokea baada ya serikali ya Kenya kutangaza kudhibiti jengo hilo zima huku hali hiyo ikishuhudiwa kwa siku ya nne.
Serikali ilisema kuwa mateka wote wameokolewa ingawa bado haijatoa taarifa rasmi kuhusu hali ilivyo sasa.
17:19 Mwandishi wa Nation TV Larry Madowo KUPITIATwitteranasema :Karibu wanajeshi kumi na wawili wako kwenye paa la jengo la Westgate wakishika. Anauliza je shughuli ya kuwasaka magaidi imekamilika?
17:15 Baadhi ya vyombo vya habari vinasema kuwa wananchi walioyaacha magari yao katika jengo hilo wametakiwa na maafisa wa usalama kwenda kuyachukua, ingawa taarifa hizo hazijathibitishwa
17:14 Milio ya risasi ilisikika mchana huu huku majeshi ya Kenya yakiendelea kukabiliana na magaidi waliosalia ndani ya jengo la Westgate. Mapema serilali ilisema kuwa magaidi sita waliuawa usiku wa kumkia leo na wengine hapo jana