Thursday, October 24, 2013

FACEBOOK YABADILI SERA.



Mtandao wa kijamii wa facebook una mpango wa kubadili sera yake ili kuwaruhusu watumiaji wake kuweza kuweka picha ambazo zina maudhui ya kutisha ambapo kama unakumbuka, May 2013
facebook ilipiga marufuku uonyeshwaji wa picha za matukio ya vurugu na mauaji pamoja na matukio yanayohusisha umwagaji wa damu na viungo vya mwili vilivyokatwa.
Sasa hivi huo uamuzi unageuzwa japo hata hivyo facebook itaruhusu watu wenye umri wa miaka 13 na kwenda mbele  kujiunga na kuweka picha za matukio kama haya lakini bado sera ya usalama ya facebook itaendelea kuzuia picha zinazoonekana kutukuza vitendo kama hivi.