Baada ya kushika sana mitaa na rekodi yake ya Ligi Soo, Msanii Rabbit aka Kaka Sungura ameamua kuugeukia uzalendo zaidi kupitia kazi yake mpya ambayo inakwenda kwa jina 1963 ‘United Kenya’ kwa ajili ya kuonyesha mapenzi na nchi yake.
Nyimbo hii maalum kwa ajili ya kuienzi nchi ya Kenya, pia ni kwa heshima ya siku ya Mashujaa iliyoadhimishwa hivi karibuni nchini Kenya na kuhudhuriwa na Rais Uhuru Kenyatta.
Huu ni muendelezo wa kazi safi kutoka kwa Rabbit ambaye ameonyesha hatua kubwa za mabadiliko na maendeleo katika muziki wake