Exclusive interview na Mr Blue Kuhusu sababu za kupotezea video ya Hemedy Phd – Rest Of My Life iliyotoka Ijumaa. Fuatilia Hapa
Blue amesema “Ni kweli Hemedy alinitafuta tufanye video ila wakati huo
nilikuwa na show nje ya nchi na nilivyo rudi sikuwa na nafasi ila
tulikubaliana kuwa tuta shoot hivi karibuni, Blue amendelea kusema
Ameshanga sana kusikia kuwa video imetoka bila yeye kuwepo na kuwa
Hemedy amechana mistari yake, Sina sababu ya kutokuwepo kwenye video ya
Hemedy kwani sisi ni marafiki na nampa heshima sana Hemedy kama kaka
yangu, Nikimuona Hemedy nitamuliza kwanini ameshindwa kusubiri mpaka
niwe na muda wa kufanya sehemu yangu na ametoa video bila mimi”
Mr Blue Alimaliza kwa kusema kuwa Atakacho
fanya ni kumtafuta na wayamalize na kama kutakuwa na version ya pili ya
hii video basi anauhakika wa kuwepo kwenye kipande chake alisema.
Baada ya kuongea na Hemedy na Mr Blue
nimegundua kuwa hawana maelewano mazuri hawa wasanii wawili kwa sababu
hakuna mwenye maelezo kamili ya issue hii na pia hapa Tanzania hakuna
msanii mwenye sababu ya msingi ya kuto onekana kwenye video ya mwenzake
unless anataka kuharibu kazi ya Mwenzake au wamegombana