Wednesday, October 23, 2013

STEVEN NYERERE AIPUA KITU.

KWA WALE WAPENZI WA BONGO MOVIE STEVEN NYERERE AIPUA KITU.
Kampuni ya utengenezaji,uuzaji na usambazi wa filamu za kitanzania Kutoka nchini Tanzania ya Proin Promotions leo imetambulisha rasmi filamu yake mpya iitwayo Long Time ambayo itapatikana kuanzia leo sokoni kwa gharama ya Shilingi Elfu tano tu za kitanzania

Filamu ya Long Time ni filamu ambayo imetengenezwa na kampuni mahiri ya Proin Promotions limited na kuigizwa na wasanii wakongwe na nguli wakiwemo Steve Nyerere, Blandina Chagula na wengine wengi.
Proin Promotions limited imejikita katika kubadilisha soko la filamu Tanzania na kuleta mapinduzi ya kweli katika tasnia ya filamu nchini,Na takribani nakala laki moja za Filamu ya Long Time zishaingia soko leo na kuuzwa.
Long Time ni filamu ambayo inafundisha na kuburudisha na pia inayoelezea Uhalisia wa maisha ya Mtanzania.